Ufisadi Air Tanzania Corp. Ltd
JK iokoe Kampuni
JK iokoe Kampuni
Sisi wananchi tuliyo ndani na nje ya ATCL tumeona hatuwezi kukaa kimya tukiangalia jinsi kampuni inavyoangamia kwa ufisadi wa kisayansi.
Ufisadi wa kisayansi kwa sababu wanaofanya ufisadi huu ni uongozi wa kampuni kwa kutumia nafasi zao za madaraka na kujifanya huo ndio uongozi.
Tuanze kwa kueleza ni maeneo gani yenye ufisadi halafu tutaje viongozi hao na sifa zao.
Tutataja maeneo yenye ufisadi na matumizi mabaya ya mapato ya kampuni na mikopo toka mabenki mbalimbali. Pia safari zilizo nyingi na za muda mrefu bila kujali gharama na faida za safari hizo. Manunuzi ya magari kwa fedha za mikopo na bila kufuata taratibu. Mwisho ni hila za kuwafukuza ama kuwaondoa katika nafasi nyeti wafanyakazi wa zamani na kuweka wapya ambao huajiriwa kiholela na bila ya sifa zinazolingana na kazi zenyewe au hata na wale waliyoondolewa.
Jopo la viongozi na sifa zao zinazoangamiza kampuni ni:-
1. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ni David Mataka. Yeye aliteuliwa na Rais JK baada ya rais aliyemtangulia kumtimua kwa ufisadi. JK alimuonea huruma DM baada ya kukaa ubaoni kwa muda na pia kushindwa kinyang'anyiro cha ubunge kwa tiketi ya chama tawala. Wananchi wa jimbo lake na wa chama chake hawakumpa kura kwa kuwa alikwisha onekana mbele ya rais BM kuwa ni fisadi wa hali ya juu japo yeye rais BM alikuwa anawakumbatia mafisadi kama Balali.
Mkuu huyu wa kampuni ameanzisha uongozi wa dharura(Management by crisis) ambapo kila asubuhi wakurugenzi na mameneja wateule katika ufisadi hukaa vikao vya kuangamiza kampuni. Amepata Benz ya kisasa katika mgao wa magari yaliyotolewa na wauzaji baada ya kununua magari ya kampuni huko Dubai kwa bei ya juu. Magari hayo ni ya mwaka 1998 japo bei yake ni karibu na mara mbili ya yale yanayouzwa na makampuni mengine ya Dubai. Yeye huwa anasuka jambo halafu anamwachia George, Eliasaph au William walichochee katika kikao cha hao viongozi.
2. Mark Manji yeye ni mtu wa Musoma japo jina lake la kihindi. Huyu ni mshauri wa mkurugenzi mkuu. Alikuwa mkurugenzi wa idara ya operations wakati wa makaburu japo idara hii huwa inaongozwa na marubani. Alipewa cheo hiki na makaburu ili kuwaweka marubani katika himaya ya makundi. Makaburu walipoondoka aliomba kuacha kazi kwa hiari na akastaafu akaomba kuendelea na kazi tena kama mshauri wa mkurugenzi mkuu. Kwa kuwa alikuwa na mapenzi na makaburu na kwa kuwa ameshapata mafao yake, hana huruma na kampuni kwa sasa badala yake yeye ni kichocheo na hujifanya analijua shirika. Anatumia utoto wa mjini kufanya kazi kwani hana shahada hata moja japo amepewa nafasi nyeti.
3. Eliasaph Mathew aliajiriwa na makaburu kama meneja wa fedha kwa maana hiyo ni mtu wa makaburu. Baada ya mkurugenzi wa fedha aliyekuwa kaburu kuondoka amekaimu nafasi hiyo hadi leo. Huyu ndie kinara wa kupindisha taratibu za matumizi ya fedha na ununuzi. Ni mfuasi namba moja wa DM kwani kwa sasa pesa za kampuni hutolewa kiholela kulipia gharama kwa ufisadi. Mfano kabla ya kufunga mwaka 2007 shillingi millioni mia mbili hamsini zilichotwa kulipa gharama za kutoa magari nane yaliyokuwa katika yadi ya kuweka mgari iliyo ya watu binafsi. Haishi hapo huchota dola elfu tatu taslimu toka kwa mtunza fedha kila mwezi na kumpa huyu mwenye yadi ya kuhifadhi magari. Huidhinisha malipo kwa ankara tu bila kujali taratibu nyingine. Ndiye aliyejumuika katika jopo lililokwenda Dubai kuchagua magari ya kampuni na kuyanunua kwa bei mbaya bila kufuata taratibu za ununuzi. Magari haya ni ya 1998 japo ATCL ni mali ya serikali,hilo halikutiliwa maanani. Yeye amepata zawadi ya VX Landcruiser ya kisasa kama mgao katika hayo manunuzi na sasa ameweka pembeni Vitara yake. Hutumiwa katika mikakati ya kuwaondoa watu wa zamani na wenye sifa kwa kuwazulia kesi na shutuma za matumizi mabaya ya pesa kitu ambacho si kweli. Waliyoonja joto hilo ni pamoja na Hassani ambaye aliamua kuacha kazi, Hamisi na Mndeme ambao wamesimamishwa kwa suala la bwana Mohamed Makaratasi ambaye ni rafiki wa George Mazula.
4. George Mazula yeye eti ndiye rubani kiongozi na mshauri wa DM. Huyu aliwahi kuachishwa kazi wakati mwenyekiti wa bodi alikuwa ni Abasi Sykes. George aliwahi kuunguza injini mbili za Fokker kwa mpigo pale Tanga. Amewahi kuangusha ndege aina ya Fokker hapa Dar es salaam. Amewahi kuua mtu pale uwanja mpya wa JK Nyerere kwa kukatwa na pangaboi baada ya yeye kuzembea kuzima injini. George ni kiungo wa mikakati yote ya ufisadi na kuondolewa watu katika nafasi zao. Alikuwa mfadhili wa DM wakati akiwa ubaoni. Ni rubani mwenye makeke na mikosi mingi. Katika dili ya Dubai yeye amepata Volvo na kujidai amekopa.
5. Amin Mziray huyu ni katibu wa kampuni. Yeye ni chapombe. Alipewa gari ya kampuni na makaburu na kulipindua kwa ulevi. Anayo shahada ya sheria lakini haitumii kwa maslahi ya kampuni. Kampuni imeshindwa kesi nyingi kwa kutokuwa makini huyu mwanasheria. Yumo katika hili jopo la ufisadi wa kampuni. Katika mgao wa magari ya Dubai yeye amepata VX Landcruiser la nguvu. Hayupo tayari kutetea hoja mbovu zinazotolewa ndani ya vikao vya hili jopo la ufisadi.
6. William Haji, anakaimu nafasi ya mkaguzi mahesabu wa ndani. Aliajiriwa wakati wa makaburu kama mkaguzi wa mahesabu wa ndani chini ya bwana Yakubu. Baada ya muda bwana YAkubu aliwekwa pembeni na huyu bwana kukaimu nafasi yake. Kwa sasa yeye ndiye anayekagua malipo (Pre-audit) hivyo yumo ndani ya mtandao wa ulaji. Ndiye anayetumiwa kutengeneza taarifa za kuzua kesi na uonevu kwa wafanyakazi wa chini. Huchukua nafasi ya afisa usalama wa kampuni ili kupindisha ukweli na hatimaye kuwadhalilisha ama kuwatimua wafanyakazi wasiyo na hatia. Ni hatari sana kwani yupo karibu na DM na Eliasaph katika kila mpango.
7. Sadiki Muze, Yeye ni mkurugenzi wa idara ya operations kwa sasa. Amepewa nafasi hiyo yeye kwani ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa DM wakati akiwa ubaoni. Pia ni mshirika wa DM katika vinywaji na mwanachama wa kijiwe kimoja na George. Ni Sadiki na George pekee waliyopewa vyeo na kuenguliwa wengine baada ya DM kuchukuwa uongozi ATCL na ni chapombe. Sadiki na George wamelipwa fadhila.
8. Heho Mbiru ni Mkenya, aliajiriwa kwa nguvu enzi za makaburu kama mkurugenzi wa masoko. Aliajiriwa kwa nguvu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya ATCL wakati huo Ali Mufuruki kwa kisingizio kuwa hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kushika nafasi hiyo. Ni mzalendo wa Kenya kweli kweli kwani kazi zinazoweza kufanyika hapa (kama Graphics) huzipeleka kwenye kampuni yake. Anayo mapenzi na makaburu hivyo kuleta mabadiliko tunayotaka yeye ni kikwazo na ndiyo maana ni rahisi kutumiwa katika hujuma. Kumbuka tunaushindani na Kenya Airways huyu atatumaliza.
9. Ajay Gopinath raia wa India. Aliajiriwa kwa nguvu wakati wa makaburu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi Ali Mufuruki. Ajay aliwahi kufukuzwa nchini lakini kwa sababu zake Ali alifanya juu chini na kumrudisha kama mkurugenzi wa mauzo. Anatumiwa katika upatikanaji wa fedha na kutumika vibaya. Hana sauti ndani ya utawala huu kwani ni mgeni.
10. Alphonse Mkinga ni meneja utumishi. Alistaafu na kuchukua mafao yake baada ya makaburu kutimka. Anafanya kazi kwa mkataba na kuzuia ajira kwa waliomaliza vyuo. Ameidumaza idara ya utumishi kwa kutoweka muundo wa utumishi na taratibu mbalimbali za ajira. Matokeo yake mkurugenzi mkuu huleta watu wake japo wapo waliofanya usaili. Mfano ni ajira ya mhudumu katika ofisi ya mkurugenzi mkuu,ajira ya afisa majengo na mali ambaye ni jamaa yake. Huyu bwana Peter Gosh anachukua nafasi ya bwana Hassan Kikoko alieandamwa na huu mtandao wa ufisadi na hatimaye kuamua kustaafu mapema. Yupo dereva aliajiriwa kwa hila japo wapo waliofanya usaili na hadi sasa hawajapata ajira. Bwana Mkinga hana sauti kwani yupo kulinda maslahi yake baada ya kupata ajira ya pili.
11. Fidelis Tarimo ni mkurugenzi wa uhandisi. Historia yake ni ufisadi mtupu. Aliwahi kusimamishwa kazi na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi wakati huo Mzee Abasi Sykes. Tarimo alikwenda kusimamia matengenezo makubwa ya Boeing ya ATC wakati huo (major check) nchini Ireland. Hakuwa anafuatilia gharama halisi za matengenezo na kujali maslahi yake hivyo kusababisha gharama kupanda kwa shilingi bilioni moja na nusu toka ghrama halisi na kulitia shirika hasara na kusimamishwa kazi. Alipata nafasi wakati wa makaburu kwani hakuwa mtetezi wa wazalendo. Kwa sasa wafanyakazi wa idara yake hawamtaki na wameandika barua ya kumkataa na wizara inajua hilo. Ni bingwa wa kuuza ndege za kampuni kwa bei ya kutupwa badala ya ile ya makubaliano ya awali. Ana ukabila na hadi sasa ana jamaa yake anasimamia ujaji wa ndege ya kukodi kwa muda mrefu yuko nje ya nchi. Ni fisadi wa kutupwa kwa ajili ya kutaka pesa za kuendeleza biashara zake.
12. Rajabu Itambo ni meneja Galileo Tanzania kampuni tanzu ya ATCL. Rajabu alipewa kazi ya ushauri katika kitengo cha Galileo na aliyekuwa meneja wakati huo Maalim Ali. Kaburu mmoja aliyekuwa mkurugenzi wa biashara Mike Bond aliamua kumuondoa Maalim Ali katika nafasi hiyo na kumuweka Rajabu kwa maslahi yake kwani walitaka kuuza Galileo kabla ya kuondoka jambo ambalo hawakufanikiwa. Mpaka sasa Rajabu ana uhasidi na wafanyakazi wa zamani kwani anataka awe mkuu wa kitengo cha ITC(Information and Technology Communication) Ni mmoja wa vibaraka wa DM.
Hadi tunakwenda mitamboni ATCL haina bajeti na hili linatokana na Eliasaph kutayarisha bajeti hiyo kwa usiri mkubwa akiweka vipengele hewa ambavyo bodi ina wasiwasi navyo hivyo kuikataa kila wakati. Bajeti huwa inatengenezwa na kitengo maalum katika idara ya fedha lakini safari hii imekuwa na usiri mkubwa. Ilibidi iwekwe hadharani kwa wafanyakazi kupitia workers council ndiyo iifikie bodi jambo ambalo halikufanyika.
Kama tulivyoeleza awali matumizi mabaya ya pesa yanapeleka kampuni kusikoeleweka. Pesa huchotwa kama za mtu binafsi bila kujali taratibu za kihasibu. Viongozi hawa kwa vikundi huenda safari kila wakati kuliko viongozi wote waliopita. Posho wanayolipana ni kubwa mno kwa kila siku hivyo hata safari za watendaji wa chini huenda wao. Mwenyekiti wa bodi Mustapha Nyang’anyi aliliambia Sunday Citizen tarehe 12 januari 2008 kuwa uzembe wa menejimenti ya ATCL kutoingia mkataba na kampuni iliyokuwa ikodishe ndege kwa ajili ya mahujaji ndiyo chanzo cha sakata zima la hasara katika usafirishaji wa mahujaji.
Ukweli ni kuwa menejimenti haikutaka kushirikisha wafanyakazi wa kawaida kuratibu safari hii kama ilvyokuwa miaka iliyopita. Hii ni kwasababu walitaka iwe siri yao kwa kutafuta ndege ya bei poa kuliko hiyo iliyopatikana kitu ambacho hakikuzaa matunda na hatimaye kusema ATCL haiwezi kusafirisha mahujaji. Mbona kabla ya makaburu iliwezekana. Hapa pana ufisadi sio uzembe tuu. Wapo wazoefu wa kazi ndani ya kampuni lakini wamekodi mtu wa nje Mtambalike rafiki yake DM kwenda kusimamia kurejea mahujaji. Tunasema hii ni hujuma na kuwadharau watendaji wa ndani.
Magari ya kampuni yamenunuliwa kwa bei kubwa bila kufuata taratibu na viongozi wanne kupata magari kutokana na gharama hiyo kubwa na bila kufuata utaratibu wa ununuzi. Hivi sasa kampuni inamadeni mengi kutokana na ufisadi. Wafanyakazi wasiotakiwa hasa wale wa zamani hutafutiwa sababu za kuwaondoa ili ajira wapewe watu wa DM. Mifano hai tumetaja hapo juu na mingine mingi tunayo kama ule wa Said Ibrahimu kufanyiwa visa na Mark Manji hadi kuamua kustaafu ili yeye Manji aongeze muda alipoamua kustaafu kwa kisingizio kuwa hakuna wa kuchukua nafasi yake.
Kwa sababu tumezungumza kwa kifupi tunaomba yafanyike yafuatayo:-
1. Kuleta wakaguzi kama vile Enerst and Young kukagua mahesabu ya ATCL tangu DM awe mkurugenzi mkuu. Hapa panatosha kuona ufisadi katika:-
(i) Mikopo na over draft na kutafuta jinsi pesa hizo zilivyotumika kwa ukamilifu.
(ii) Kupata maelezo kutoka kwa DM kwa nini toka achukue uongozi ATCL hakubadilisha muundo na uongozi wa makaburu tukijua fika viongozi hao wana maslahi na makaburu.
(iii) Uchunguzi juu ya ununuzi wa magari bila kufuata kanuni na taratibu za ununuzi nje ya nchi na kulinganisha bei na makampuni mengine ya Dubai
(iv) Wachunguzwe hawa viongozi wanne walipataje magari hayo toka kwa kampuni iliyouza magari kwa ATCL kwa bei ya juu. Kama ni mikopo waoneshe pesa walipata wapi na utaratibu mzima wa kuyalipia na kuingiza na kuyakomboa.
(v) Zipatikane sababu za viongozi kuomba kustaafu na kujiajiri tena.
(vi) Uchunguzi ufanywe kupata uhalali wa wafanyakazi wa zamani kunyanyaswa na wengine kusimamishwa kazi kwa hila ili kuajiri wengine kwa maslahi ya uongozi.
(vii) Uchunguzi ufanywe kuhusu malipo yote kwenye kampuni iliyohifadhi magari toka yatolewe bandarini.
(viii)Uchunguzi ufanywe kuhusu elimu na uwezo wa Peter Gosh kwani aliyeondolewa kwa hila alikuwa Civil Engineer.
(ix) Uchunguzi ufanywe kuhusu safari zote walizosafiri hawa viongozi kama zilileta manufaa. Wamesafiri sana na pesa nyingi zimetumika. Kuna wakati menejimenti yote ilikwenda China kwa pamoja japo waliondoka kwa vikundi.
(x) Mwisho serikali ichukue hatua mapema kabla kampuni haijaangamia. Sisi tuliopo nje na ndani tunaona na tunajua, na kama kutahitajika msaada tupo tayari kutoa ushirikiano.
Chanzo cha habari: Jambo Forums
No comments:
Post a Comment