Nusu fainali
Wamisri wawaaibisha
Wa´ivory Coast
Wa´ivory Coast
Misri 4
Ivory Coast 1
Ivory Coast 1
Wa´ivory Coast wakicheza mpira wa kiufundi "display football" na karibu kuwazidi Wamisri "The Pharaohs" kila seksheni ya uwanjani walijikuta wakitolewa kwenye nusu fainali, baada ya kuaibishwa kwa kufungwa magoli 4 - 1. Misri walipata goli la kwanza dakika ya 12 ya mchezo kwa bao lililofungwa na Ahmed Fathy. Mpaka kipindi cha kwanza kinakwisha, Misri walikuwa wanaongoza kwa goli moja kwa bila. Misri ilipata goli la pili dakika ya 62 lililofungwa na Amr Zaki. Ivory Coast hawakukata tamaa, walicheza kabumbu la uhakika, dakika ya 63, Abdelkader Keita alipiga bomba toka mbali na kuipatia Ivory Coast goli. Misri wakicheza kwa mashambulizi ya kuvizia na aina ya "effective football", walipata goli la 3 dakika ya 67 lililofungwa na Amr Zaki. Dakika ya 91, Misri ilipata goli la 4 lililofungwa na Mohamed Aboutrika. Kipa wa Misri, Al Hadar alifanya kazi kubwa. Alidaka na kupangua mashambulizi matano ya wazi, ambayo yangeweza kuwapata Ivory Coast ushindi!
Timu zilikuwa hivi:
Ivory Coast: Barry (Loboue 37), Boka, Toure, Eboue, Meite, Toure Yaya, Zokora, Kalou (Bakari Kone 60), Drogba, Dindane (Arouna Kone 79), Keita. Marizevu: Tiassa Kone, Djakpa, Fae, Gervinho, Gohouri, Romaric, Sanogo, Tiene, Zoro.
Goli: Keita dakika ya 63.
Misri: El Hadari, Mohamed, Hany Said, Fathy, Hassan, Moawad (Fathallah 77), Gomaa, Abd Rabou, Aboutriaka, Moteab (Zidan 69), Zaki (Ibrahim Said 86). Marizevu: Sobhy, Abdel Monssef, El Mohamady, El Saeed, Fadl, Gamal, Mostafa, Shaaban, Shawky.
Magoli: Fathy dakika ya 12, Zaki dakiza za 62, 67, Aboutriaka dakika ya 91.
Watazamaji (Kumasi) 30,000
Refarii: Eddy Maillet (Seychelles).
Kipa wa Ivory Coast, Boubacar Barry aliumia na kutoka, nafasi yake ilichukuliwa na Stephan Laboue. Drogba akimsaidia Barry kutoka.
No comments:
Post a Comment