Wasifu mfupi wa
Alisoma katika shule mbalimbali kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1971, ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) mwaka 1974.
Kuanzia mwaka 1974 hadi 1978, Pinda alifanya kazi katika Wizara ya Sheria, akiwa Mwanasheria wa Serikali.
Mwaka huo huo wa 1978, Pinda alihamia katika Ofisi ya Rais, ambako alifanya kazi kama Ofisa Usalama wa Taifa hadi mwaka 1982.
Pinda hakuishia hapo, mwaka 1982 hadi 1992, alifanya kazi kama Katibu Myeka Msaidizi wa Rais, akiwa msaidizi wa karibu wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, kwa miaka saba na mrithi wake, Alhaj Ali Hassan Mwinyi,
Mwaka 1996 hadi 2000, alifanya kazi kama Katibu wa Ikulu katika Baraza la Mawaziri.
Mwaka 2000 alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Mpanda Mashariki na mwaka huo huo, akateuliwa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), chini ya Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2005.
Ni katika kipindi hicho ambacho Pinda alionyesha uwezo mkubwa katika utendaji wake, akijibu maswali yote magumu yaliyoelekezwa kwa wizara yake na wabunge mbalimbali.Pengine ni kutokana na uzoefu huo, ndiyo maana Rais Kikwete akaamua kumrejesha katika wizara hiyo alipounda Baraza la Mawaziri Januari 2006, lakini safari hii yeye akiwa ndiye bosi wa wizara hiyo iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Ameishikilia nafasi hiyo hadi juzi, wakati Rais Kikwete alipovunja Baraza la Mawaziri na kisha kumteua kuwa Waziri Mkuu wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pinda ni mtoto wa kwanza kwa wazazi wake, ambao wote bado wako hai. Amejaliwa kupata watoto watatu—wote wa kike. Watoto hao ni Narusi, Mkalo na Edwik.
Waziri Mkuu mteule Mizengo Pinda akiliutubia bunge jioni hiii mara baada ya uteuzi wake kupitishwa kwa kura 279 (98.9)''
-Nanukuu
"Mimi ni mtoto wa Mkulima"
"Ni mtoto wa kwanza kuzaliwa"
"Wazee Kijijini watashangaa"
Hivi sasa wabunge wanaunga mkono hoja kaanza Hamad Rashid Mohammed kasifia saana akafuata Edward Lowassa naye kasifia ile mbaya, akafuatana mama Getrude Mongela amesifu mpaka sijui vipi.Sasa wanazungumza Anna Abdallah, atazungumza Zitto Kabwe na wengineo.
Bunge la jamhuri la muungano wa Tanzania limempitisha aliyekua waziri wa Tamisemi Mh Peter Mizengo Pinda kuwa waziri Mkuu wa Tanzania kwa kura 279(98.9)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda anakuwa Waziri Mkuu wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitanguliwa na Julius .K.Nyerere, Rashid Kawawa, Cleopa Msuya, Edward Sokoine, Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, John Malecela, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa.
Waziri Mkuu mteule ataapishwa kesho saa tano kamili asubuhi ikulu ya Chamwino mjini Dodoma,Baraza la mawaziri linatarajiwa kutajwa siku ya jumatatu wiki ijayo na kuapishwa siku jumatano..
No comments:
Post a Comment