Kizimbani kwa
kumlawiti mtoto
na julian msacky
MKAZI wa Magomeni, Ismail Singano (20) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 10.
Kesi ya mtuhumiwa huyo ilikuwa inasikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam jana na Hakimu Mkazi, John Lemboko, ambapo upande wa Mashitaka uliongozwa na Inspekta wa Polisi, Thomas Mtikatika.
Inspekta Mtikatika alidai katika kosa la kwanza, mtuhumiwa bila uhalali wo wote alimbaka mwanafunzi huyo Januari 29, mwaka huu eneo la Magomeni Mapipa. Mwendesha Mashitaka huyo alidai katika kosa la pili, mtuhumiwa alimwingilia kinyume na maumbile mwanafunzi huyo ambaye jina na shule yake vimehifadhiwa katika mwezi huo eneo la Magomeni Mapipa, katika Wilaya ya Kinondoni.
Inspekta Mtikatika alipomuuliza mtuhumiwa kama alihusika kumbaka na kumlawiti mwanafunzi huyo wa darasa la tatu, alikana shitaka hilo.
Mtikatika alidai upelelezi dhidi ya makosa yanayomkabili mtuhumiwa haujakamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.
Hakimu Lemboko alisema dhamana ya makosa aliyotenda mtuhumiwa ipo wazi.
Alisema masharti ya dhamana ni kwa mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili wenye kazi zinazotambulika.
Lemboko aliahirisha kesi ya mtuhumiwa huyo hadi Februari 19, mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment