Wanatafuta utajiri kwa
kutoajiri wenye sifa za ajira
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
MIMI sitaki ugomvi Bwana. Itakuwaje unishakie kwa kila mtu eti kwa kuwa niko mbali na wewe? Eti yule rafiki yako aliyekuja wiki jana alisema nimezidi kunawiri na kupendeza. Nifanye nini? Nichanjechanje uso wangu? Eti ameona wageni wa bosi wananiangalia na macho ya uchu. Wewe hujui maisha yetu sisi wasichana?
Tukijijitokeza tu mbele ya macho ya wanaume wanadhani kazi yetu ni kuwagawia chochote tulicho nacho. Ndiyo! Hata marafiki wa bosi wananitongoza. Cha ajabu ni nini? Unafikiri wewe peke yako umeona kwamba angalau ninapendezapendeza? Labda mimi nashangaa wanaume. Yaani, hawawezi kumwacha msichana apite bila kumwaga sera kama radhi. Lakini unajua hii si hoja. Hoja ni je! mimi nakubali au nakataa? Siwezi kuzuia kutongozwa lakini naweza kukataa. Na nakataa daima!
Bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment