


Mvua kali na radi zilifanya kipindi cha kwanza kuwa si cha kusisimua. Kila timu ikicheza kwa uoga na uangalifu. Hadi dakika 45 za kwanza kwisha matokeo yalikuwa sifuri kila timu. Hispania walianza kwa mashambulizi mara tu baada ya filimbi ya kipindi cha pili kupulizwa. Dakika ya 50 walipata goli la kwanza lililofungwa na Xavi Hernández. Baada ya goli hili, Hispania walicheza kwa kupeana pasi za uhakika na za kiustadi sana kiasi cha kuwafanya Warusi wakimbize mpira uwanja mzima! Goli la pili la Hispania lilifungwa na Daniel Güiza dakika ya 73. Goli hili liliwavunja Warusi moyo. David Silva aliwapa Hispania tiketi ya fainali, baada ya kufunga goli la tatu kwenye dakika ya 82.
Fainali Jumapili 29 Juni 2008 kati ya Hispania na Ujerumani
No comments:
Post a Comment