Wednesday, June 11, 2008


Kundi A

Uswisi yaaga fainali

dakika za majeruhi

Uturuki 2 = Uswisi 1

Wakicheza nyumbani na kwenye mvua kali, kwenye uwanja wa St. Jakob Park mjini Basel, Uswisi wametolewa kwenye fainali za mataifa ya Ulaya baada ya kufungwa magoli 2 – 0 na Uturuki. Uswisi ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli kwenye dakika ya 32 lilifungwa na Hakan Yakin (Mswisi mwenye asili ya Uturuki). Uswisi walienda kwenye mapumziko wakiwa wanaongoza kwa golii hilo. Goli lakusawazisha la Uturuki lilifungwa na Sentürk Semih kwenye dakika ya 57. Goli la ushindi la Uturuki lilifungwa kwenye dakika ya 92 (dakika za majeruhi) na Turan Arda. Uswisi wanacheza mechi ya mwisho kwenye kundi hilo na Ureno tarehe 15 Juni. Hata kama watawafunga Ureno, bado hawatakuwa na nafasi ya kusonga mbele.


Hakan Yakin (Uswisi) akishangiliwa na wenzake baada ya kufunga goli


Semih Şentürk (Uturuki) akishangilia goli la kusawazisha

Ureno 3 = Chekia 1

Mechi ilikuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja wa Stade de Geneve. Ureno wakicheza kwa uhakika na kujiamini, walifungua mlango kwenye dakika ya 8 kwa goli lililofungwa na Deco baada ya kazi kufanywa na Christiano Ronaldo na Nuno Gomes. Chekia hawakukata tamaa. Walifunga goli la kusawazisha kwenye dakika 17 lililofungwa na Sionko.Goli la pili la Ureno lilifungwa na Christiano Ronaldo baada ya mapumziko kwenye dakika ya 63. Goli la tatu la Ureno lilifungwa na Quaresma dakika ya 90.


Kapteni Nuno Gomes akimpongeza C. Ronaldo baada ya kufunga goli.


Scolari kuikochi Chelsea!

Luiz Felipe Scolari, kocha wa Ureno. Scolari ameingia mkataba na Chelsea kuifundisha timu hiyo kuanzia Julai Mosi.




No comments: