Kuvaa nguo za ndani
za mtumba
ni kujidhalilisha?
Na Editha Majura
MIAKA ya karibuni, Serikali kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ilipiga marufuku biashara ya nguo za ndani za mtumba, na bidhaa hiyo ilitoweka kabisa kwa kipindi fulani.
Soksi, sidiria na chupi ndiyo mavazi yanayohusishwa na zuio hilo kwa lengo la kulinda utu wa mtu na kuiepusha jamii na matatizo ya kiafya yanayohofiwa kuwa yanaweza kutokana na matumizi ya mavazi hayo.
Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni biashara hiyo imeibuka tena na inashamiri kwa kasi huku baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam wanaonunua bidhaa hiyo wakifurahia hali hiyo.
Jambo la kujiuliza ni kwa vipi mamlaka yenye dhamana ya kuainisha na kudhibiti ubora wa bidhaa nchini itoe tahadhari dhidi ya bidhaa lakini jamii inayotetewa ionyeshe kutoridhishwa na tahadhari hiyo?
Bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment