Tunahitaji: Wendawazimu
wa Anne Kilango
TUMEMSIKIA bungeni Mheshimiwa Anne Kilango akizungumza kwa uchungu juu ya ufisadi. Ametaka fedha za EPA zilizochotwa na mafisadi zirudishwe kwa wananchi.
Ametoa mfano wa Socrates, mwanafalsafa wa Uyunani ya kale aliyekuwa tayari kufa kwa kusimamia anachokiamini. metamka bungeni kuwa yuko tayari kufa kwa anachokipigania. Hakika hayo aliyozungumza ni maneno mazito.
Mheshimiwa Mbunge Anne Kilango
Ujasiri wake huo ni kuwa na kiwango fulani cha ‘wendawazimu’, kitu ambacho Watanzania tunahitaji kuwa nacho. Tuyaseme yale muhimu yanayotakiwa kusemwa hata kama tutaonekana ni wendawazimu. Kwa staili yake na kipaji cha kuzungumza alichojaliwa, Anne Killango mara nyingi ameweza kuwasilisha ujumbe wake kwa lugha ya kawaida na yenye kueleweka kwa wananchi. Hata kama kuna wanaomwandama kwa anayoyasema, lakini wananchi wa kawaida, na walio wengi, wanamwelewa Anne Killango, anazungumza kile ambacho wangetaka kizungumzwe.
Bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment