Sunday, July 27, 2008



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.

Mpenzi Frank,


VIPI mpenzi wangu? Yaani ninavyokaa mbali na wewe nakumic kuliko maelezo. Nilalapo nakumbatia mto nikijaribu kujidanganya nakukumbatia wewe.

Niamkapo na kujikuta peke yangu kitandani, naumia roho vibaya sana hadi natupa mto. Na ni hapo tu natamani itokee miujiza uibuke papohapo. Hata kumwomba Mungu namwomba ingawa najua haiwezekani.

Najua pia utanicheka mpenzi wangu maana ujinga huo haupendi kabisa. Lakini ni kwa sababu ya kukumic tu, na hata hivyo, nitakuwa nina tofauti gani na Watanzania walio wengi? Si uliwasikia wale ambao walipiga kambi uwanja wa ndege bila pesa wala pasi, bila tiketi wala kibali cha kufika majuu eti Mungu kawatuma kwenda Ulaya?


No comments: