Saturday, July 26, 2008



Nchi kamili..

Serikali ya mapinduzi

Zanzibar yasema!!!!


*Yasisitiza ni nchi, muda wa kudhibitiana umepita
*Shamhuna, Raza wahoji nafasi ya Tambwe ndani ya CCM
*FIFA yapigilia msumari yasema haiitambui kama nchi


Na Ali Suleiman, Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesisitiza kwamba Zanzibar ni nchi kamili na itaendelea kuwa hivyo na zama za kutishana na kutaka kudhibitiana katika hilo, zimepitwa na wakati.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri Kiongozi, Bw. Ali Juma Shamuhuna, wakati akijibu hoja mbali mbali za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochangia makadirio ya matumizi ya Wizara ya Habari, Utangazaji na Michezo kwa mwaka wa fedha 2008/9.

Wajumbe wa Baraza waliochangia makadirio hayo walitaka kusikia tamko la SMZ katika suala hilo, ambalo limekuwa mjadala mkubwa uliotawala hivi sasa nchini.

Bw. Shamuhuna alisema alikemea vitisho vinavyotolewa na baadhi ya watu wakitaka mjadala huo kusitishwa na wengine kusema kujadili suala hilo ni sawa na uhaini.

"Nani wa kuwadhibiti wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika suala hili ... enzi za vitisho na kutaka kudhibitiana zimepitwa na wakati, suala hili waachiwe Wazanzibari wenyewe kulijadili," alisema Bw. Shamuhuna.


No comments: