Wednesday, July 23, 2008


Mawaziri

wa Muungano

wamepotosha



*Yachachamalia kauli za Khatib na Sumari

Na Ramadhan Haji, Zanzibar

WIZARA ya Fedha na Uchumi Zanzibar, imesema maelezo yaliyotolewa bungeni Dodoma hivi karibuni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Bw. Muhammed Seif Khatib na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Jeremiah Sumari ni ya upotoshaji yasiyo na ukweli wowote.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Wizara hiyo jana, ilisema Serikali ya Muungano haijawahi kutoa mgao wa misaada ya kibajeti inayopelekewa kwa njia ya mikopo kwa SMZ na badala yake mikopo hiyo imekuwa ikitolewa na Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na washirika wengine wa maendeleo.

"Tunaomba msaada wenu vyombo vya habari ili kuelezea ukweli wa jambo hili, ambalo linaweza kupotosha wananchi kwa kuwa kilichosemwa na waheshimiwa hao hakiendani na ukweli wenyewe, ni vyema kutoa taarifa hii kwa umma ili kusahihisha taarifa zilizotolewa awali," ilisema taarifa hiyo.


No comments: