
Waliompekua Chenge
LONDON, Uingereza
TAASISI inayoshughulika na uchunguzi wa ufisadi, Serious Fraud Office (SFO) imekabidhi ripoti yake ya mwaka huku ikiweka hadharani mambo mbalimbali na kesi ilizokumbana nazo katika kipindi cha mwaka mmoja.
SFO ndio ile taasisi isiyo na mzaha (serious) iliyokuja nchini kumpekua aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kabla ya kwenda nchini Uingereza katika Kisiwa cha Jersey ambapo ilikuta amechimbia sh bilioni moja kwenye akaunti yake binafsi, fedha ambazo inadaiwa alizipata kwa dili chafu ya uuzaji wa rada ya kijeshi.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kwenye tovuti ya taasisi hiyo, ripoti hiyo ya kuanzia mwaka 2007 hadi 2008 ilikabidhiwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu mpya wa taasisi hiyo, Richard Alderman ambaye alichukua wadhifa huo mwezi Aprili mwaka huu.
Akikabidhi ripoti huyo mkurungezi huyo mkuu mpya, pamoja na mambo mbalimbali alizungumzia changamoto zilizoikabili SFO katika kipindi cha miaka 29 tangu taasisi hiyo ianze kufanya kazi zake za kiuchunguzi na mafanikio yaliyofikiwa na taasisi hiyo katika kufichua ufisadi na kulinda mali za umma.
No comments:
Post a Comment