Ubabe wa udume ni utumbo
matumbo
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
Vipi mpenzi? Nafurahi sana kuona umeacha wivu wako wa uovu maana umeniumiza sana hakuna maelezo. Yaani nakuambia nimepata homa ya ghafla kutokana na tuhuma zako zisizo na kichwa wala miguu.
Tena uniambie faraja ya maisha yangu, tangu lini udumae na mfumo dume!! Mimi nakujua unawacheka sana watu wote wanaona ukubwa wa misuli au ukali wa kauli ndiyo uanaume. Iweje uingie hapa na wewe, mpenzi wangu?
Eti kama ninafanya maasi nitakutambua. Mbona nakutambua sana tumaini langu? Mbona wakati wote natamani kudunduliza vijisenti vya kutosha tuweze kuanza maisha yetu pamoja?
No comments:
Post a Comment