Wednesday, July 02, 2008

'Wanaotaka Mugabe

ajiuzulu wakajinyonge

mara 1,000'



SHARM EL-SHEIKH, Misri

RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe hatajiuzulu na wale hususan wa Mataifa ya Magharibi wanaoubeza uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo hivi karibuni wakajinyonge, Msemaji wa Rais huyo alisema jana.

Kiongozi huyo wa Zimbabwe alikuwa hapa akihudhuria Mkutano wa Kawaida wa 11 wa Umoja wa Afrika (AU) uliomalizika jana.

Viongozi katika mkutano huo hawakuwa tayari kumpinga Rais Mugabe hadharani na badala yake kwa chinichini walikuwa wakishinikiza Rais huyo akubali kugawana madaraka na Upinzani.

Msemaji wake, Bw. George Charamba alipinga katakata mapendekezo ya kugawana madaraka. Baadhi ya viongozi walionesha kutoridhishwa kwao na shinikizo alililowekewa Rais Mugabe wakisema ni dhaifu.


Bofya na endelea>>>>>

No comments: