Red Bull yasimamishwa
Kuuzwa Ujerumani:

Majimbo 6 nchini Ujerumani yamesimamisha uuzaji wa kinywani maarufu cha kuongeza nguvu kiitwacho Red Bull, baada ya kugundulika kina miligram 0.4% ya cocaine. Majimbo hayo ni: Hesse, North Rhine-Westphalia, Thuringia and Rhineland-Palatinate. Uchunguzi ulifanywa kwenye jimbo la Nordrhein-Westfalens. Kiwango cha asilimia 0.4 kilichogundulika ni kidogo sana kwa madhara ya binadamu, lakini kutokana na sheria za Ujerumani, ni marufuku kinywani au chakula cha aina yoyote kuwa na madawa ya kulevya, msemaji wa wizara ya afya, wa jimbo la Thuringia, Bw. Thomas Schulz ameiambia Deutsche Welle.
No comments:
Post a Comment