Tuesday, May 19, 2009

Ida the Missing Link

amebadili historia

ya mwanadamu







Mwanasayansi Dk. Jørn Hurum akiongoza wanasayansi wa Kinorwejiani wa Idara ya Historia za Kale, Chuo Kikuu cha Oslo Norway wametangaza chanzo cha binadamu mjini New York leo kwenye Makumbusho ya Historia ya kale (American Museum of Natural History). Mabaki kamili ya mwili wa kamnyama hako yamepewa jina la ”Ida”, (jina la mtoto wa Jørn Hurum) au Darwinius masillae kwa kitaalamu kwa ukumbusho wa sehemu aliyofukuliwa mara ya kwanza na ukumbusho wa miaka 200 ya kuzaliwa kwa Charles Darwin.

Kufuatia maelezo ya wanasayansi hao, ”Ida” ni kiungo kilichokosekana cha chanzo cha binadamu (Missing Link) ambacho kimekuwa kikitafutwa na wanasayansi kwa karne kadhaa, kitabadili historia ya binadamu. Mabaki ya ”Ida” yana miaka milioni 47 (arobaini na saba)

Mabaki ya ”Ida” yaligunduliwa sehemu inayoitwa Messel Pit karibu na Darmstad nchini Ujerumani kwenye Kiangazi cha mwaka 1983. Kwa miaka mingi mabaki hayo yalikuwa kwenye makumbusho ya mtu binafsi. Baadaye huyo mtu akawasiliana na dalali mmoja anayejulikana kwa jina la Thomas Perner. Perner naye akawasiliana na Dk. Hurum. Hurum na idara yake walimnunua "Ida" kabla hata ya kumwona kwanza. Inasemekana Chuo Kikuu cha Oslo kilimnunua "Ida" kwa Dala milioni moja za Kimarekani.

"Ida" (Darwinius masillae) ana urefu wa sentimita 53, na alikuwa mtoto wa miezi 6 hadi 8 na ni msichana.

Dk. Jens Franzen, mwanasayansi bingwa wa maeneo ya Messel Pit, anasema ”Ida” ni kama maajabu ya nane ya dunia, kwa maajabu ya kupatikana na viungo vyake vilivyo kamili. 

No comments: