Mumeo ana mwanamke nje,
utajuaje?
Sasa skia, najua unataka uhakika, zifuatazo ni dalili 12 kujua kuwa mumeo ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine badala yako.
1. Kwanza utaona tu ghafla matumizi yake ya fedha yanakuwa juu... kuna mwanamke anamgharamia shosti, kaa hapo.
2. Anakutafutia visa bila sababu za msingi mgombane mara kwa mara... jua anatafuta sababu ya kuhalalisha tamaa yake ya kuwa na mwanamke mwingine. Hii mara nyingi wanaitumia wanaume ili wasionekane wakosaji.
3. Hataki kuulizwa alikuwa wapi, huenda ukimuuliza anakuja juu. Hapa tayari unaona tofauti na zamani alipokuwa akikuaga au kukubembeleza.
4. Utaona akirudi tu nyumbani anakimbilia bafuni kuoga, hataki kufanya chochote... hataki kupoteza muda kuongea... moja kwa moja bafuni. Huko shoga anaenda kujipoza moyo kwa maovu anayokutendea.
5. Ghafla ameanza kuwa makini katika vaa yake... anahakikisha amependeza kabla ya kutoka nyumbani na huenda akawa amenunua nguo mpya nyingi kwa idadi isiyo yakwaida yake au bila ulazima. Shosti shtuka kuna mtu anataka kumpendaza huyo.
6. Mume amekuwa bize! muda mchache anautumia na wewe.
Anatafuta kila sababu kukukwepa, huenda akawa anachelewa kurudi nyumbani kuliko kawaida yake na anaondoka mapema zaidi kwenda kwenye mihangaiko yake. Huyu shoga si mwenzako.
7. Hapokei simu yako, na wala hakupigii baada ya kuona miss call yako. Ujue anajihisi muovu kuongea na wewe akiwa anakufanyia mabaya. Inawezekana pia akawa anazima simu na visingizio vya charge vikawa vingi. Ghafla hamna mawasiliano mazuri kama zamani.
8. Hajiamini tena na simu yake. Anazima simu akiingia tu nyumbani, au labda huwa anaizimia huko huko nje. na kama haizimi basi utaona yuko bize anajibu msj. Simu ikiingia anaongea kama mtu mwenye haraka ya kuikata.
9. Hataki ushike simu yake, hajisikii vizuri ikiwa mikoni mwako. Huenda akawa ameiweka namba ya siri. heee!
10. Umegundua kuna namba nyingi ambazo huzijui, kila siku ya Mungu namba fulani zinajirudia na huenda ukawa umezitilia mashaka baadhi ya namba hizo. Uko sawa kabisa kuna tatizo hapo...!
11. Hashiriki kikamilifu katika tendo la ndoa. Inawezekana pia akawa hakutamani tena kama zamani. Hakufurahii. Mmmmh, hapo kuna alama ya hatari shosti.
12 Anakuuliza uko wapi kila wakati, wakati anajua utakuwa wapi. Unadhani anajali kumbe mwenzako anatafuta namna ya kukuibia vizuri. Hapo anajitahidi kuwa muangalifu, au kwa lugha nyingine watoto wamjini wanakwambia... Mwizi Smart.
Haya shosti... Kama kwa namna yoyote ile vitu kama hivyo anavifanya jua unauhakika wa asilimia mia moja kuwa anakutenda. Lakini bado muda wa kumwambia kuwa unajua kila kitu haujafika.
- Na Asmah Makau
Kutoka gazeti la Mwananchi mtandaoni
No comments:
Post a Comment