Wednesday, July 29, 2009

Serikali ya Mapinduzi


yakiri Wapemba wengi kutoandikishwa





Vigogo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wamekiri kuwa idadi kubwa ya watu walikwama kuandikishwa katika daftari la wapiga kura kisiwani Pemba kutokana na kutokuwa na vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi.

Vitambulisho hivyo wameshindwa kuvipata kutokana na kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa na hivyo kupoteza sifa za kusajiliwa kama Wazanzibari Wakaazi.

Hayo yalielezwaa na wakuu wa mikoa miwili ya Pemba walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar jana.

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi alisema serikali haina nia ya kumyima mtu haki yake ya kikatiba, isipokuwa inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia katiba na sheria ya uchaguzi ya Zanzibar.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa alisema kumejitokeza tatizo kwa baadhi ya Wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara na nchi za Uarabuni kurejea kisiwani Pemba wakitaka kuandikishwa katika daftari hilo, kitendo ambacho alisema ni kinyume na katiba ya Zanzibar kwani mhusika anatakiwa awe ameishi kwa miaka mitano mfululizo.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba, Juma Kasim Tindwa, alisema chama cha CUF tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa kimekuwa kikifanya udanganyifu kisiwani Pemba na kufanikiwa kunyakua majimbo yote ya uchaguzi.

CHANZO: NIPASHE

No comments: