Ripoti ya kijarida cha Cheche za Fikra juu ya Meremeta imekamilika. Ina kurasa karibu 50 ikiambatanishwa na vielelezo lukuki ambavyo kwa wengi itakuwa ni mara ya kwanza kuviona hadharani, vielelezo ambavyo serikali yetu na baadhi ya wanasiasa mafisadi imefanya jitihada kubwa kuhakikisha havioni nuru ya siku kwa muda mrefu.
Ndani ya ripoti hii maswali kadhaa yanajibiwa kwa kina (mengine kwa kupita tu). Yanajibiwa si kwa ufundi wa hoja na uzuri wa ushawishi wa maneno bali kwa ushahidi mzito na vielelezo ambavyo vyenyewe peke yake vinatosha kabisa kufunga mjadala huu.
Tunaamini kuwa kama sisi Watanzania hatutasimama na kupinga mambo ya uovu yanayofanywa kwa jina letu basi watawala wetu wataendelea kufanya maovu kwa jina letu. Tunafuata mfano wa Wamarekani waliofichua na kukasirishwa na Ab Ghraib au Waisraeli waliojitokeza kupinga vitendo vya jeshi lao dhidi ya Wapalestina. Tunaamini kwenye uovu, hakuna uzalendo wala undugu – there is no patriotism in the presence of evil! ….. bofya na angalia:
Wednesday, July 29, 2009
Siri za Meremeta mtandaoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment