Friday, July 24, 2009

Ubelgiji kutoa msamaha

kwa watu wanaoishi

isivyo halali nchini humo

Mfano wa pasi ya Kibelgiji


Wiki hii bunge la Ubelgiji limepitisha muswada utakaotoa msamaha kwa watu wanaoishi isivyo halali nchini humo. Kuanzia Septemba 15 hadi Desemba 15, watu wote ambao wanaishi isivyo halali wanaweza kujitokeza na kuomba vibali vya kuishi nchini humo. Msamaha huo unawahusu watu ambao wamekaa nchini humo si chini ya miaka mitano.


Waziri mkuu wa Ubelgiji, Herman Van Rompuy.


Hayo yalisemwa jana na waziri mkuu wa Ubelgiji, Herman Van Rompuy. Rompuy amesema kuwa mtu ambaye ameishi miaka miwili na nusu na muda wote huo amekuwa akifanya kazi, pia anaruhusiwa kuomba kuishi kihalali.

Gazeti la kila siku nchini humo, De Standaard limeandika kuwa msamaha huo unaweza kukusanya watu 50 000 (hamsini elfu) watakaojitokeza. Inasadikiwa kuna watu 100 000 (laki moja) wanaoishi isivyo halali kwenye nchi hiyo.

Nchi za Ulaya ambazo zimewahi kutoa msamaha kwa waliokuwa wakiishi isivyo halali:

Italia – toka mwaka 1982, imetoa msamaha kwa watu milioni moja na nusu

Ufaransa – kati ya 1997 na 1998 ilitoa msamaha kwa watu 80 000 (themanini elfu).

Ubelgiji – mwaka 2000 ilitoa msamaha kwa watu 30 000 (thelathini elfu).

Hispania – mwaka 2005 ilitoa msamaha kwa watu 60 000 (sitini elfu).

Sweden – mwaka 2005 ilitangaza kuwa watu waliokuwa wanaishi isivyo halali wajitokeze, walijitokeza watu 8000 (elfu nane) kutaka kuomba msamaha. Lakini serikali ya Sweden ilishtuka, kwani haikutegemea kuwa watu wengi kiasi hicho walikuwa wakiishi isivyo halali. Wengi walioomba, walinyimwa.

Uholanzi – mwaka 2007 ilitoa msamaha kwa watu 30 000 (thelathini elfu).


1 comment:

Anonymous said...

WANORWEJIANI BASI NA WAO WANGETOA MSAMAHA. SIDHANI KAMA HAPA NORWAY KUNA ZAIDI YA WATU 5000 WANAOISHI BILA MAKARATASI.