Friday, August 07, 2009

Kama una simu soma hii!



Watumiaji wa simu za mikononi nchini wamehadharishwa kuwa makini na simu au ujumbe mfupi wanaopokea kutoka kwa watu wasiowajua.

Hadhari hiyo ambayo imetolewa na msamaria mwema katika mitandao ya intanet inaeleza kuwa ikiwa utapokea simu kutoka kwa mtu yeyote akidai kuwa yeye ni fundi wa kampuni husika au kwamba wanashughuhlikia laini yako ya simu na kukutaka kubonyeza # 90 au #09 au namba nyingine yoyote, unahadharishwa kuikata simu hiyo haraka.

Msamaria huyo anadai kuwa watu hao hutumia vifaa ambavyo pindi unapofuata maelekezo yao huwawezesha kupiga simu kwa kutumia gharama zako.

Chanzo: Dar Leo

No comments: