Friday, August 07, 2009

Sotomayor aweka historia

Kwenye mahakama kuu ya Marekani



Bi. Sonia Sotomayor akifurahia kukubaliwa kuwa jaji wa mahakama kuu ya Marekani.


Baada ya wiki kadhaa za mvutano kikao cha juu cha Bunge la Marekani (Seneti), Bi. Sonia Sotomayor, amepitishwa kuwa jaji wa mahakama kuu ya Marekani. Bi. Sotomayor anakuwa Mmarekani wa kwanza kwenye asili ya Latini Amerika kwenye mahakama kuu. Alipitishwa kwa kura 68 na 31 zilimpinga. Wazazi wa Sotomayor walihamia Marekani toka Puerto Rico na amekulia kwenye hali ya umaskini kitongoji cha Bronx mjini New York. Baba yake alifariki akiwa na miaka 8. Mama yake ambaye alikuwa nesi, alijikaza kufanya kazi zaidi ya moja ili kuhakikisha watoto wake wanakuwa na kupata elimu, na Sonia Sotomayor ametimiza ndoto za mama yake.


No comments: