Fainali za kombe la Afrika
(Africa Cup of Nations)
zinaanza kesho nchini Angola
Kuanzia Jumapili 10. Januari 2010 hadi Jumapili 31. Januari 2010
Fainali za 27 za kombe la Afrika zinaanza kesho nchini Angola. Kutakuwa na jumla ya mataifa 16, Angola ikiwa mwenyeji wa mashindano.
Jana timu ya taifa ya Togo, ilishambuliwa kwa bunduki rashasha na wanamgambo wapinzani wa jimbo la Cabinda nchini Angola. Togo walikuwa wakisafiri kwa basi kutokea Kongo Brazaville, kuelekea Cabinda kwenye mechi yao ya kwanza. Dereva wa basi hilo aliuawa na wachezaji wawili kujeruhiwa. Mchezaji wa kiungo wa Togo; Alaixys Romao akihojiwa na vyombo vya habari alisema kuwa: wachezaji wa Togo wameathiriwa kisaikolojia na wanafikiri kuwa watashindwa kuhimili purukushani za fainali kwa sababu ya tukio hilo la kigaidi.

Mpaka sasa shirikisho la soka la Togo ( Fédération Togolaise de Football), halijatoa taarifa rasmi kufuatilia tukio hilo. Timu ya Manchester City anayochezea Emmanuel Adebayor imetoa taarifa kuwa mchezaji huyo mzima na yuko fiti, pia Aston Villa anakochezea Moustapha Salifou wamesema kuwa mchezaji huyo ameshtushwa na tukio lakini yuko fiti.
Togo wanatarajiwa kukwaana na Ghana kwenye mechi yao ya kwanza kama wataamua kuendelea mashindano haya.
Mataifa ya Afrika yanayoshiriki kwenye fainali hizi za mwaka huu:
Angola
Ghana
Ivory Coast
Tunisia
Algeria
Misri (Egypt)
Cameroon
Gabon
Nigeria
Mali
Benin
Burkina Faso
Msumbiji (Mozambique)
Zambia
Togo
Malawi
No comments:
Post a Comment