Saturday, January 09, 2010

Mwanasoka Bora Afrika wa BBC


Didier Drogba, mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa BBC Afrika.



Didier Drogba wa Chelsea na Ivory Coast ametangazwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa BBC Afrika 2010.
Mshambuliaji huyo amepata kura zaidi kuliko Samuel Eto'o, Michael Essien, Yaya Toure, na Tresor Mputu Mabi kushinda taji hilo.
Matokeo ya kura - zilizopigwa na mashabiki kote Afrika yalitangazwa moja kwa moja kutoka Angola kupitia kipindi cha Fast Track katika Idhaa ya Kiingereza ya BBC.
Drogba yupo Angola akiiongoza nchi yake kujiandaa kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, ambako The Elephants wanapewa nafasi kubwa ya kushindwa.
Baada ya kuanza mwaka vibaya, Drogba aliimarisha kiwango chake cha soka na kuwa mmoja wa washambuliaji tishio duniani.
Baada ya kuwekwa kando kucheza kikosi cha kwanza na kocha Luis Felipe Scolari kutoka Brazil, mshambuliaji huyo alifunga goli moja tu katika mechi 10 ilipofika Februari.

Waliowahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika
2008 - Mohamed Aboutrika
2007 - Emmanuel Adebayor
2006 - Michael Essien
2005 - Mohamed Barakat
2004 - Jay-Jay Okocha
2003 - Jay-Jay Okocha
2002 - El Hadji Diouf
2001 - Sammy Kuffour
2000 - Patrick Mboma

Chanzo: BBC Swahili

No comments: