Baada ya masaa na wasiwasi mwingi hatimaye Mkurugenzi wa
Uchaguzi amemtangaza Bw. Joshua Nassari (CHADEMA) kuwa Mbunge mteule baada ya
kumshinda Siyoi Sumari wa CCM. Bw. Nassari alitoa mojawapo ya hotuba za
kusisimua kutolewa baada ya ushindi. "Tulianza na Mungu, Tutamaliza na
Mungu" amesema Mbunge huyo ambaye ni miongoni mwa wabunge vijana zaidi
nchini.
1 comment:
CCM tukae tukijua kuwa kuna vyama vya upinzani makini sasa si mchezo! Tuliwapeleka wazito wote tukaogopa kumpelekea mwenyekiti wetu Kikwete manaake ingekuwa aibu.
CHADEMA sasa onyesheni upevu angalieni makosa yenu jisahihisheni na nawatakia kila la heri.
Kama alivyosema Nape Mnauye baada ya matokeo kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.
Wana CCM tukubali tumezidiwa kete na CHADEMA Arumeru.
Tuwe makini na watu kama hawa wanaotukana saa zote. Ikiwezekana tuwaondoe. Kuna vijana wengi CCM wenye uwezo wa kuzungumza bila kutukana!!!
MwanaCCM Mdemokrasia wa kweli
Post a Comment