Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni an Michezo, Daniel Nsanzugwanko alisema hivi karibuni: "Katika kuhakikisha tunadumisha utamaduni wetu, tunaandaa waraka ambao utakuwa unawataka walimu kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia shule za sekondari. Waraka huo tunataajia kuupeleka kwa mawaziri ukapitiwe haraka."
Aidha, alisema kwamba maandalizi ya awali yanaendelea vizuri, na tayari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeandaa kitabu chenye maneno yote ya Kiswahili na tafsiri yake ya Kiingereza.
Kwa mujibu wa Nsanzugwanko, wote wanaokibeza Kiswahili ni washamba. Alisema Kiswahili ni lugha inayojulikana kwa sasa, na inatumiwa na watu zaidi ya millioni 180 duniani kote.
Chanzo: http://www.wanafunzi.or.tz/habari_zote.php
No comments:
Post a Comment