Sunday, September 02, 2007

Stars yainyoa Uganda moja


Mashabiki wa timu ya taifa ya soka "Taifa Stars"


Taifa Stars


Timu ya taifa ya Uganda "The Cranes"


Patashika kati ya Taifa Stars na the Cranes


Mashabiki kibao walijaza uwanja mpya wa soka jijini Dar.



Hata watoto nao walikuwepo "Neshno Stedium"
Picha zote zimepigwa na Muhidin Issa Michuzi


Uwanja mpya wa taifa. Wadau mnasemaje ukiitwa
Ben Stadium? Kwa heshima wa Rais Mtahafu, Benjamin
William Mkapa? Kwani aliahidi kuwa angejenga uwanja
wa kisasa kabla ya kwisha uongozi wake, na alitimiza ahadi.

Picha zote na habari za juu toka:
http://issamichuzi.blogspot.com/


2007-09-02 11:00:58
By Jimmy Charles

Bao pekee liliwekwa kimiani na kiungo mshambuliaji, Abdi Kassim `Babi` jana liliitoa kimasomaso timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Yosso wa Uganda, The Cranes, uliofanyika kwenye uwanja mpya na wa kisasa jijini Dar es Salaam.

Bao hilo liliwekwa kimiani na `Babi` katika dakika ya 54 katika mchezo huo wa kuiandaa Stars kupambana na Msumbiji utakaofanyika Jumamosi ijayo jijini Dar es Salaam kusaka tiketi ya kwenda Ghana mwakani kucheza fainali za Mataifa ya Afrika.

Abdi alifunga bao hilo kwa shuti kali akiwa nje ya 18 baada ya kugongeana vizuri na Said Maulid na Haruna Moshi, katika mchezo huo uliokuwa na kila aina ya burudani.

Mchezo huo mbali na kuipima Stars kabla ya kukwaana na Msumbiji, Black Mambas, pia ulikuwa maalum kwa ajili ya kuuzindua uwanja huo mpya wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 waliokaa.

Hata hivyo, washambuliaji wa Stars kama wangekuwa makini wangeweza kuibuka na ushindi wa mabao mengi, lakini licha ya kupata nafasi nyingi walishindwa kufunga mabao kufuatia kutokuwa makini.

Stars: Ivo Mapunda, Mecky Mexime, Amir Maftah, Nadir Haroub, Salum Swed, Henry Joseph, Nizar Khafan, Shabaan Nditi, Haruna Moshi, Said Maulid na Abdi Kassim.

Uganda: Hannington Kalyesubula, Simon Masaba, Richard Malinga, Peter Makanga, Musa Doka, Johnson Bagole, Daniel Wagaluka, Patrich Ochieng, Yuda Mgalu, Hamis Kitagenda na Mike Seruma.

  • SOURCE: Lete Raha

No comments: