Thursday, February 28, 2008

Wacha nikusekese na

KiSwahili....




BABY WHAT'S YOUR NAME: Perth Zoo has named its new rothschild giraffe, Mapenzi, which means ''much loved'' the Swahili language. Picture: Richard Polden


Ingali ule ugonjwa wa kudandia KiSwahili na majina ya KiSwahili inaendelea ukiwa unaendelea, huko Australia amezaliwa twiga waliyempa jina "mapenzi".

IT'S official, Perth Zoo's eight-week-old giraffe has a name - Mapenzi, which in the east African Swahili language means "much-loved''. Mapenzi, a female calf, is the first giraffe born at the zoo for seven years. (endelea kujisomea mwenyewe hapa)
Hilo tuliache, twende kwenye kiseko kya leo,Rubani mmoja katika eneo la Kenya, alikuwa na WaKenya katika shughuli zao za kawaida. Yeye alijifanya kuwa anakifahamu KiSwahili, hakuhitaji darasa.

Wewe utakubaliana nami kuwa kwa lugha ya Kiingereza mtu unaweza kuagiza, chicken legs, chicken wings, chicken glizards nk.Sasa hiyo siku, rubani na wenyeji wake wamefika hotelini kwa maakuli ya mchana, ilipofika muda wa kuagiza chakula, rubani akasema, 'nataka kuku matiti...'!
Ama si kicheko hiko bali balaa. Alipotakiwa kuwa makini na kuacha utani, akarejea sentensi ile ile. Basi ndipo walipomwomba ajieleze kwa Kiingereza ambapo alisema, '....chicken breast and ... '.(kisa hiki amenisimulia rafiki Rebecca Wanjiku)

Jamani, kujifunza lugha ya watu muhimu ama kama vipi, basi kaa kimya tu labda iwe unakufa njaa na hata na hivyo, si unon'gone na mwenyeji ama si uulize?Makubwa!


By

Subi'



No comments: