Wednesday, February 27, 2008



Watakiwa kujihadhari na makahaba


Na Waandishi Wetu, Morogoro

WANAUME wametakiwa kujihadhari na wanawake wanaofanyakazi ya kujiuza baada ya kuibuka mtindo wa kupaka matiti dawa za kulevya na kuwalewesha wateja wao na kisha kuwaibia.

Kutokana na kuibuka kwa mtindo huo umewaliza wanaume wengi wanaofuata huduma kwa wanawake na kujikuta wakiibiwa kila kitu baada ya kulewa na kupitiwa na usingizi mzito.

Imefahamika kuwa changudoa hao hupaka dawa za kulevya kwenye matiti na kwamba mwanaume akinyonya matiti hayo hulewa na kujikuta akiamka asubuhi akiwa ameibiwa kila kitu.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai mkoani Morogoro, Ahmed Msangi amesema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakiibiwa kwa mtindo huo na kuogopa kutoa taarifa.

Amesema uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa wanaume wanaofuata huduma ya mapenzi kwa changudoa hao hufanyiwa vitendo hivyo.

Msangi amesema wanaume hao wamekuwa wakiogopa kutoa taarifa kwa kuogopa kuharibu ndoa zao.

Amesema mpango wa kuwakamata changudoa hao utaweza kufanikiwa endapo wanaume wanaofanyiwa vitendo hivyo watatoa ushirikiano kwa polisi.

"Ili changudoa hao waweze kukamatwa ni vizuri wanaume wanaofanyiwa vitendo hivyo wakatoa taarifa polisi badala ya kuona aibu, " amesema.

No comments: