Laana ya mwaka!!!
Na Imelda Mtema, Mkuranga
Hii ni laana! Wakazi wa Kijiji cha Mwalusembe kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, wanadai kushangazwa na familia moja iliyopo kijijini hapo kwa madai baba mwenye nyumba na mkewe wanafanya ngono na watoto wao.....
Chanzo chetu cha habari kilitupasha kuwa, sakata la familia hiyo kwa baba kula mayai yake na mama pia kuwavulia nguo wanawe wa kiume, lilianza muda mrefu lakini lilizimwa kimyakimya, huku wazee wa kijiji wakiamua kutumia busara zao kurekebisha mambo.
Mpashaji wetu alidai baba wa familia (jina tunalihifadhi kwa sasa) ndiye aliyeanza tabia hiyo chafu ya kufanya mapenzi na binti zake na kuna siku alifumwa na mkewe (jina tunalo) akivunja amri ya sita akiwa na mwanawe.
Inadaiwa mke alitishia kuondoka ndipo mumewe alipoomba msamaha na kuahidi kutorudia tena kitendo hicho, huku mama mwenye nyumba akikubali kwa sharti la mzee huyo kutowasogelea binti zake.
“Mzee (akimtaja jina) hakukoma, kwani baada ya muda alihamia kwa mtoto wake mwingine aliyekuwa anasoma na kuanza kufanya naye mapenzi, kitendo hicho kilimkasirisha mkewe ambaye aliamua kumshawishi mtoto wake wa kiume nao wazini,” kilisema chanzo chetu.
Mwandishi wa habari hizi alipofika kijijini hapo ili kujua hali halisi, baadhi ya wanakijiji walikiri kuwepo kwa tukio hilo na kudai linawakera kwani inaonekana kama ni laana kwao.
Aidha, mzee anayetuhumiwa kutembea na wanawe wa kike, alikana kuwepo kwa kitu hicho na kudai kuna hali ya kumuonea wivu, kwani huo uvumi unasambazwa na wasiomtakia mema.
Mkewe naye alikataa kutokea kwa tukio hilo la wao kutembea na watoto wao, huku akisisitiza ni majungu ya watu wasiopenda kuona maendeleo yao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwalusembe, Manzi Mkomo alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alikiri kulisikia lakini akadai halijafikishwa mezani kwake kushughulikiwa kwani ni suala la kifamilia zaidi.
“Hili ni suala la kifamilia na inaonekana limemalizwa na wao wenyewe, lakini nimesikia kuwepo kwa tukio hilo ila sijui kama ni kweli, kwani sijalithibitisha zaidi ya kusikia maneno yaliyozagaa hapa kijijini juu ya tukio hilo, “ alisema.
Kutoka gazeti la Ijumaa, 28 Machi 2008

No comments:
Post a Comment