Na Imelda Mtema
Mke wa mwanamuziki wa dansi nchini Muumini Mwinjuma, Chiku Kasika amekunywa sumu kwa nia ya kutaka kujiua, kwa kile kilichodaiwa ni baada ya kunyimwa talaka na mumewe....
Akizungumza na Ijumaa, mtoa habari kwetu alisema Chiku alikunywa sumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa nyumbani kwake Tandale kwa Mtogole, Dar es Salaam.
Shuhuda wetu alitupasha kuwa, mara baada ya kunywa sumu kulisikika mikoromo hali iliyosababisha majirani kuvamia nyumbani kwake na kumkuta akigaagaa chini kwa maumivu.
Chanzo chetu kinasema, majirani hao kuona hivyo waliamua kukodisha teksi na kumkimbiza katika Hospitali ya Mwananyamala, alipofikishwa madaktari walianza kuhaha ili kuokoa maisha yake.
Mtoa habari kwetu alidai kuwa, kwa muda mrefu sasa, Chiku alikuwa anadai talaka baada ya kuchoshwa na mienendo isiyoridhisha ya mumewe ambayo kwake aliona kama inamdhalilisha.
Chanzo chetu kilidai kuwa, Muumini aligoma kutoa talaka kwa kile alichoona jamii itamfikiria vibaya kutokana na kitendo chake cha kuoa na kuacha kila mara. Kwa Muumini Chiku ni mke wake wa tatu.
Baada ya Muumini kugoma kutoa talaka, inadaiwa Chiku alikasirika na kuamua kununua sumu ya panya na kunywa, kabla ya majirani kumuwahi na kumkimbiza Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam ili kuokoa maisha yake.
“Chiku ameshachoka na mambo ya Muumini ndiyo maana aliamua kudai talaka na aliponyimwa aliamua kunywa sumu,” kilisema chanzo chetu.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika Hospitali ya Mwananyamala na kumkuta Chiku amelazwa katika Wodi na. 15, huku akiwa hoi na amewekewa dripu.
Alipoulizwa kiini cha yeye kunywa sumu, alianza kulia kwa sauti kubwa huku akidai kuna matatizo makubwa yaliyomsababisha achukue hatua hiyo.
“Samahani sana dada yangu acha tu ni matatizo makubwa ndugu yangu, nitakapojaliwa kutoka ndio nitaeleza vizuri kila kitu,” alisema Chiku huku akilia.
Muumini alipoulizwa kuhusu hilo, alitupa lawama na kudai anashangaa anafuatwa yeye kwani kuna watu wengi wanafumaniwa lakini hawaandikwi.
“Mimi kama mke wangu kanywa sumu mngemuuliza yeye mwenyewe, lakini mimi sina jibu labda mngeniuliza mafanikio yangu tu ndiyo ningewajibu.”
Habari tulizozipata wakati tunaenda mitamboni zinasema Chiku aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo juzi Jumatano.

No comments:
Post a Comment