Wednesday, June 04, 2008

Sakata la Sammy Korir:

Mapolisi waliomwajiri

wasimamishwa kazi!



Sammy Kipterer Korir


Baada ya skandali ya polisi kumwajiri Sammy Korir kama kachero wao wa kuchunguza Waafrika nchini Norway kuandikwa kwenye gazeti la Dagbladet, mapolisi wawili wa kitengo cha polisi kinachoshughulikia wageni, wamesimamishwa kazi na uchunguzi unafanywa dhidi yao. Huenda wengi kwenye kitengo hicho, wakasimamishwa kazi, kufukuzwa kazi hata kushtakiwa.

Dagbladet la leo linaandika kuwa, Korir alikuwa analipwa mshahara, huku hao mapolisi waliomwajiri wakiaandika kuwa analipwa posho ya ukalimani.

Jana Dagbladet liliandika jana kuwa kijana mmoja, Emmanuel Agara alirudishwa Ghana, licha ya kusema kuwa kwao ni Liberia. Kwa uongo wa Korir, Agara alirudishwa Ghana mara mbili. Mara zote hizo mbili, polisi wa Ghana walikataa kumpokea Agara na kuwaambia polisi wa Norway waliomsindikiza Agara kuwa jamaa si Mghana na warudi naye Norway.

Mara ya pili Polisi wa Norway waliomsindikiza Agara walimtelekeza uwanja wa ndege wa Accra, na wakaingia mitini, lakini polisi wa Ghana walimrudisha Agara Norway.

Habari zaidi zinasema, Korir alikuwa anajisifu na kuwaambia watu wasimchezee na kuonyesha hicho kitambulisho cha polisi alichopewa na hao mapolisi mafisadi.


Chanzo cha habari: Gazeti la Dagbladet.



No comments: