Maandamano
Kuwa

Ni nchi yaruhusiwa
na Mwanne Mashugu, Zanzibar
HATIMAYE maandamano ya kupinga kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa Zanzibar si nchi, yameruhusiwa kufanyika kwa masharti mazito Zanzibar.
Maandamano hayo yatafanyika keshokutwa, Agosti 10, baada ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mjini, Mkadam Khamis Mkadam, kutoa kibali cha kufanyika kwa maandamano hayo.
Kwa mujibu wa barua ya polisi yenye kumbukumbu namba W/MJN/SO.7/2/A/106 ya Agosti 7, ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, maadamano hayo yatafanyika kuanzia katika viwanja vya Kombawapya hadi Kibandamaiti, ambako kutakuwa na mkutano wa hadhara.
Polisi katika barua hiyo walisema, watahakikisha ulinzi unakuwepo kuanzia mwanzo wa maandamano hadi mwisho.
“Haturuhusu kuchukua mabango ya aina yoyote, hususan yanayozungumzia hadhi ya Zanzibar ni nchi au si nchi,” ilisisitiza barua hiyo ya polisi.
No comments:
Post a Comment