Mjadala wa
na hadithi ya wavuvi
HAIKUWA nia yangu kuandika makala juu ya suala la ‘Zanzibar si nchi’. Binafsi siamini kama ni suala limeibuka tu hivi hivi. Na madhari suala hili lina harufu ya ajenda fulani iliyojificha tunaolijadili hatuna budi kuwa waangalifu.
Kama nilivyokwisha kueleza huko nyuma tayari wapo watu wanaolijadili suala hili kwa kutumia mioyo yao badala ya fikra. Wengine wanalijadili kwa kutumia mawazo ya waganga wa kienyeji na wapiga ramli. Wapo pia wanaolijadili kwa kuangalia maslahi binafsi ya mtu, kikundi, chama, na kadhalika. Wanaweka kando maslahi ya wananchi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla!

No comments:
Post a Comment