Saturday, August 16, 2008

Serikali yatoa onyo

Yapiga marufuku

maandamano



na Nasra Abdallah

SERIKALI imesema mgomo uliopangwa kufanywa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), ni batili na watakaothubutu kushiriki watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alisema mgomo huo ni batili kwa kuwa haukufuata taratibu.

Waziri huyo alisema ili waweze kugoma, wafanyakazi hao wangepaswa kwanza kupeleka malalamiko yao kwenye baraza la majadiliano.

“Kama majadiliano hayo yatashindikana kutolewa majibu katika baraza hilo, wangetakiwa kutoa notisi ya siku 60 kabla ya mgomo, jambo ambalo hawajalifanya,” alisema Ghasia.


No comments: