Uraia wa nchi mbili
UNAPOONA kichwa cha habari kinafanana na kichwa cha wiki iliyopita, usidhani kwamba makala hii imerudiwa. La hasha. Ni mwendelezo wa makala ile, unaotokana na maoni, maswali na hoja mbalimbali zilizotolewa na wasomaji. Wengi waliandika kupitia tovuti ya gazeti hili na mwingine alinipigia simu. Wengi wa waliotoa maoni yao, wamenilaumu kwa kutokuwa na ufahamu juu ya faida za uraia wa nchi mbili. Wengine walifikia hatua ya kunieleza kuwa sina ufahamu wa kutosha kuhusu suala la uraia na kupendekeza nirudi kwa mwalimu wangu wa darasa la kwanza ili nikajifunze tena.
Kwa huyu ningependa kumpa changamoto ndogo tu. Kama aliona kuwa sina uelewa wa suala hili, ni kipi alikiona katika makala ile kilichomsukuma kutoa maoni yake? Kwangu mimi, inaniwia vigumu sana kutoa maoni kuhusu kitu nisichokielewa, hivyo, labda yeye ndiye hakunielewa.
No comments:
Post a Comment