Sunday, September 07, 2008

Mama ndevu!!!



Na Dunstan Shekidele, Morogoro.

Muhudumu mmoja wa baa maarufu ya Pema iliyopo eneo la Lunna mkoni hapa, aliyefahamika kwa jina moja la Asha, ambaye amejaliwa na mola kuwa na ndevu nyingi kama mwanaume, ameamua kutozinyoa ndevu hizo na kuziachia bila hiyana.

Mwandishi wetu, mwishoni mwa wiki hii, alimshuhudia mwana mama huyo akipiga kazi bila noma yoyote ambapo baadhi ya wateja wageni walionekana kumshangaa.

Alipotakiwa kuzungumzia uamuzi wake wa kitozinyoa ndevu hizo, Bi Asha alijibu kwa mkato kwamba yeye ni mke wa mtu na kwamba suala ya kuziacha ndevu hizo ni uamuzi wake na mumewe. Baa ya Pema ni miongoni mwa baa maarufu mkoni Mororgoro na zinozopendwa na mapedeshee wengi wa mkoa.

Kutoka Global Publishers Tanzania


No comments: