Wednesday, September 17, 2008


Sheikh adaiwa

kubaka ndani

ya mwezi

Mtukufu wa

Ramadhani


Rhobi Chacha na Amina Salim

Sheikh wa madrasa ya Istiqama ya Toroli Chang’ombe, Dar es Salaam, anayejulikana kwa jina la Sheikh Matogolo, anadaiwa kumbaka msichana wa miaka 12, anayesoma darasa la 5 katika Shule ya Msingi Unubini jijini ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Tukio hilo la kusikitisha, limedaiwa kutokea hivi karibuni Chang’ombe Toroli ambapo sheikh huyo, amedaiwa kuwa na tabia ya kumwingilia kimwili binti huyo, (jina tunalihifadhi) kwa muda mrefu sasa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho tunakipa hifadhi ya jina lake, wakati sheikh huyo akiendeleza tabia hiyo chafu, wazazi wa binti hawakuelewa chochote, hadi siku za hivi karibuni waliposikia kutoka kwa majirani kuwepo kwa mchezo mchafu wa kimapenzi kati ya sheikh huyo na binti yao.  




1 comment:

Anonymous said...

astaghafilullah!!!!