Unataka kuwa
Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Norway,
Forsvaret Etteretningstjeneste
(Norwegian Intelligence Service),
linatafuta watu wa kuwa majasusi. Tangazo hilo la kazi liko
kwenye tovuti ya shirika hilo. Tangazo hilo limetolewa
Septemba tano.
Vigezo vya kuomba kazi hiyo ya ujasusi:
* Mwombaji awe na elimu ya juu
* Mwombaji awe na leseni ya gari daraja B
* Mwombaji apasi uchunguzi wa afya
* Mwombaji apasi vikwazo vya hali ya
juu vya kiusalama
* Mwombaji awe raia wa Norway
Mwombaji anatakiwa kutuma maombi:
LUKS/LSES,
Flyplassveien 300
1590 RYGGE.
Ili maombi ya mwombaji yafikiriwe, mwombaji:
* Aandike sababu za kwa nini anataka kuwa jasusi
* Aambatanishe na CV na kopi zilizothibitishwa kuwa ni kopi
sahihi za shahada, vyeti vya kozi mbalimbali na majina
na anwani za watu si chini ya wawili wa
kumthibitisha (kumkinga kifua)
* Aandike wasifu wake
* Aambatanishe picha 2 za rangi
Maombi pia yanaweza kutumwa kwenye faksi namba:
69 23 77 49.
Kopi za vyeti na maombi havitarudishwa kwa
mwombaji hata kama hakukubaliwa.
Mwisho wa kutuma maombi ni: 3 Oktoba 2008
Kwa habari zaidi, mwombaji anaweza kupiga simu:
69 23 77 41.
Tangazo hilo unaweza kulisoma kwa Kinorwejiani kwenye:
No comments:
Post a Comment