Amri ya 11 ya Mungu:
‘Msitaje bure majina
matukufu ya
waheshimiwa
wabunge wenu.’
ABDUL Rahman Mohamed Babu, katika kitabu chake, ‘African Socialism or Socialist Africa?’ (Tanzania Publishing House, 1981) aliandika ukurasa wa 165 kwamba, serikali katili huogofya zaidi kuliko chui.
Alikariri insha ya Bertrand Russel, aliyewahi kuandika kisa cha mwanamke aliyekutwa ubavuni mwa Mlima Thai, akilia kwa uchungu jirani na kaburi.
Mwanamke yule alipoulizwa, kwa nini aliomboleza kwa uchungu namna ile, akasema ni kutokana na uchungu na huzuni kubwa ndani ya huzuni:
‘Kwanza,’ mama yule akasema, ‘Baba wa mume wangu aliraruliwa hapa na chui, kisha mume wangu akauawa hivi, sasa mwanangu naye kauawa kwa jinsi hii hii.’
Akaulizwa, ni kwa sababu gani alikuwa hajaondoka mahali pale yasije kumkuta yaliyowakuta watu wake, akasema ‘Hakuna serikali katili hapa!’ bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment