Wednesday, November 19, 2008



Waziri awamu ya

tatu na ya nne kortini


* Vigogo zaidi wachanganikiwa matumbo moto 
* Tahadhari nzito zachukuliwa dakika za mwisho 

Na Mwandishi Wetu, Dar Leo Jumanne jioni 18.11.2008

WAZIRI mmoja mwandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu ambaye pia alifanya kazi katika Awamu ya Nne chini utawala wa Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kufikiwa mahakamani leo katika Sakata la kukomba mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) 

Habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa waendesha mashitaka katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisuti jijini Dar es Salaam zinasema kuwa alipata taarifa za kuletwa kwa waziri huyo(jina tunalo) mahakamani jana lakini suala hilo liliahirishwa dakika za mwisho. 

Hata hivyo wakati tukienda mitambo, taarifa zinasema huenda waziri huyo akafikishwa mahakamani hapo mchama huu. 

Taarifa hizo hazikufafanua zaidi kuwa waziri huyo atafikishwa mahakamani hapo kusomewa makosa gani. 

Kufikishwa kwa kigogo huyo kutafungua sura mpya ya sakata hilo. Baadhi ya watu wamedai kwamba hatua hiyo inaweza kuwa mwanzo mbaya wa kuingia kwa msururu wa vigogo kwenye sakata hilo. 

"Tunaamini akiletwa mengi yatafumka, sakata hili litachukua sura mpya, huenda ndio maana tahadhari kubwa inafanyika katika utekelezaji wake. Wengi matumbo moto" kilisema chanzo chetu.

No comments: