Thursday, November 20, 2008

EPA: Kama vile

mchezo wa kuigiza


WAKATI baadhi ya watuhumiwa wakiwa wamekwisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), mbinu chafu zilizotumika na vigogo katika kuchota mabilioni ya fedha katika akaunti hiyo sasa zimebainika.

Mbinu hizo ni pamoja na kughushi nyaraka mbalimbali na kutumia kivuli cha siasa katika kupitisha nyaraka husika bila kufanyika kwa uhakiki wa kina wa uhalali wa nyaraka hizo, kazi iliyofanyika kwa kasi iliyowashangaza hata wakaguzi wazalendo na wale wa kimataifa waliopitia hesabu za BoT.

Mfano wa dhahiri uliotolewa tokea mwanzo ni ule wa kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, ambayo ilithibishwa tokea mwanzo jinsi vigogo walivyoghushi nyaraka za kampuni 12 za kigeni kuweza kujichotea kiasi cha Sh bilioni 40.....bofya na endelea>>>>>


No comments: