Aliyemlawiti mwanawe
atupwa jela miaka 60
Mkazi wa Msalato, Augustino Letema Slau (45), amehukumiwa kwenda jela miaka 60 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumlawiti mwanawe wa kumzaa mwenye umri wa miaka 10.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya mkoani hapa, Groly Mwakihaba alidai mahakamani hapo jana kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Septemba na Novemba mwaka jana, ambako katika muda usiojulikana, alimwingilia mwanawe kinyume cha maumbile na kumbaka.
Hakimu huyo alisema katika eneo la Msalato katika Manispaa ya Dodoma, mtuhumiwa huyo alimbaka mwanawe na kumlawiti ambapo baada ya kufanya kitendo hicho, alimtishia mtoto huyo kuwa iwapo atasema atamnyonga hadi afe.
Mwakihaba alisema wakati Sau akimwingilia mwanawe, alikuwa akimpaka mlenda katika sehemu zake zote za siri jambo ambalo lilimsababishia maumivu makali.
Alisema mtoto huyo aliyekuwa akilala na shangazi yake baada ya mama yake mzazi kufariki, alikuwa akichukuliwa na baba yake huyo na kumpeleka chumbani kwake muda ambao walikuwa peke yao na kumvua nguo zake na kuanza kumfanyia vitendo hivyo huku akimwonya kuwa asimweleze mtu yeyote.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa baadaye walimu wa mtoto huyo walimwona akiwa anatembea vibaya huku akiwa mnyonge, kitendo kilichowalazimu kumhoji, ndipo alipowaeleza kuwa baba yake amekuwa akimlazimisha kumbaka na kumlawiti.
Alisema baada ya walimu hao kupata maelezo hayo, walimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitali ya Serikali ya Mirembe ambako mtoto huyo alifanyiwa uchunguzi wa kina na kubainika kuwa alikuwa amefanyiwa vitendo hivyo.
Hakimu Mwakihaba alisema taarifa ya daktari ilibainisha kuwa mtoto huyo alikutwa ameharibika katika sehemu yake ya uke huku sehemu yake ya nyuma ikiwa imeongezeka ukubwa na kuingia vidole viwili tofauti na ilivyo kawaida, jambo ambalo lilionyesha kuwa mtoto huyo ameingiliwa mara nyingi.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi ikiwamo mtoto huyo, unamtia hatiani mtuhumiwa na kuhukumiwa miaka 30 kwa kila kosa; la kwanza likiwa ni kufanya mapenzi na mtoto wake na kosa la pili likiwa ni kumlawiti, vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria na adhabu hiyo ataitumikia kwa pamoja.
Awali, Mwendesha Mashitaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Christina Mkonongo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo kutokana na vitendo hivyo kukithiri katika jamii ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo. Naye mtuhumiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa aliiomba mahakama isimtie hatiani kwa kuwa hakufanya vitendo hivyo na kuwa hayo ni majungu tu ambayo yamefanywa kwa ajili ya kutaka kumwangamiza.

No comments:
Post a Comment