Kikwete akilegea
CCM imekwisha
MKUTANO Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unafanyika baadaye wiki hii, Dodoma, huku chama hicho kikikabiliwa na mgawanyiko mkubwa pengine kushinda yote iliyopata kuwapo huko nyuma, na hofu ya kujitokeza kwa kura za itifaki kama ilivyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2002, wachunguzi wamesema.
Kimsingi mkutano huo utahitimisha uchaguzi ambao umekuwa ukiendelea ndani ya chama hicho ambao nao unatajwa kuwa chanzo cha mgawanyiko wa dhahiri hasa baada ya kuwapo tayari mgawanyiko katika maeneo mengi katika ngazi za wilaya na mkoa.
Tayari CCM imekwisha kupata uongozi wake toka chini hadi ngazi ya mikoa unaoingia ndani ya Halmashauri Kuu (NEC). Unaosubiriwa kufahamika pamoja, ndio unaotarajiwa kukiendesha chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano hadi mwaka 2012.
Habari za ndani ya CCM ambazo Raia Mwema imezipata zinasema kwamba kuna mabadiliko ya kiutaratibu yaliyofanywa na vikao vya juu vya CCM ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kupiga kura katika makundi ya mikoa badala ya kwenda mbele katika masanduku isipokua kwa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu wake..............bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment