Wednesday, December 31, 2008

Mama Salma Kikwete:

Atinga TBC 1

Na kuendesha kipindi



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (pichani) hivi karibuni amefanya kali ya mwaka na kuwashangaza wabongo baada ya kutinga katika studio za Kituo cha Televisheni cha TBC1 na kutangaza kipindi cha watoto. Mama Salam aliendesha kipindi hicho mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa na wanafunzi kutoka shule ya msingi Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, ambao aliwauliza maswali mbalimbali wanafunzi hao walioonekana kujawa na furaha.

Katika kipindi hicho, mke huyo wa mheshimiwa rais alikuwa akiwasomea wanafunzi hao kitabu cha hadithi kilichotungwa na kijana mmoja aitwaye Edward kinachoeleza tabu alizozipata alipokuwa mtoto wa mitaani hadi alipopata malezi katika kituo cha kulelea watoto cha Dogodogo Center cha jijini.

“Jamani watoto wazuri mnajua maana ya kutweta? Kama hamjui niangalieni mimi ninavyofanya (anawaonyeshwa wanafunzi hao jinsi ya kutweta) si mmeniona watoto wazuri ninavyofanya? Huku ndio kutweta,” alisema mama Salma. Hata hivyo, uendeshaji wa kipindi wa mwanamama huyo ulionesha kuwavutia wengi waliobahatika kukiona huku baadhi wakitamani awe anakiendesha kila siku.

“Mimi kwa kweli nilishangaa kumuona Mama Salma akitangaza tena kwa umahiri mkubwa ila nikawa najiuliza kwamba, kuna uwezekano kweli wakwawa wamemuajiri kabisa? Hilo sijui lakini kusema kweli hata mimi mtu mzima nilivutiwa na kipindi hicho,” alisema Mama Winnie mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Kutoka Global Publishers Tanzania


No comments: