Thursday, December 04, 2008


Nawashangaa watu wazima

kwa wazimu wao wa

kushindwa kutambua

uzima wetu



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,

VIPI switii, umetua na mvua?  Usiwe umevuta blanketi chapa mtu eti baridi imezidi.  Tena wiki hii kumekuwa na siku ya UKIMWI kwa hiyo usije ukamsherehekee UKIMWI kwa kumkaribisha nyumbani.  Maana mpenzi majambozzz na mavituzzz ya siku hizi … si unajua tena!

Na sisi tulisherehekea UKIMWI vilevile.  Bosi akatupeleka kwenye sherehe yenyewe.  Mwaka huu sherehe yote ilikuwa yake.  Yeye ni Waziri wa Mikiki na Makeke na hakuna gonjwa kama UKIMWI kuleta mikiki na makeke.  Basi yeye alikuwa mgeni rasmi na bila shaka alitaka kuonyesha anavyotamba.

Lakini mimi kwanza nilishangaa.  Kwa nini watoto na vijana wanatumika kama pambo tu.  Mara waimbe nyimbo, mara wacheze igizo.  Watu wanapiga makofi, wengine wanawasifia kama vile wanashangaa kwamba watoto na vijana wana mawazo yao.  Kama ni hivyo, kwa nini wanatupeleka shule kama si kutuwezesha kutumia akili zetu.  Na tunapotumia akili hizi wanashangaashangaa.  Mimi kwa kweli nawashangaashangaa watu wazima kwa wazimu wao wa kushindwa kutambua uzima wetu...bofya na endelea>>>>>


No comments: