Jenerali Nkunda
Jenerali Laurent Nkunda, kiongozi wa kikundi cha waasi, Mashariki ya Kongo amekamatwa jana Alhamisi saa 4 na nusu za usiku na majeshi ya Rwanda akijaribu kutoroka kutoka Kongo kuingia Rwanda. Wiki hii Rwanda ilituma kikosi cha wanajeshi 4000 kwenda kuisaidia Kongo kukabiliana na Jenerali Nkunda.
Kukamatwa kwa Jenerali Nkunda kunaonyesha kubadilika kwa siasa kwenye eneo hili, kwani Nkunda, ambaye ni Mtutsi, alikuwa ni swahiba wa Rais wa Rwanda, Jenerali Paul Kagame (Mtutsi) tokea kumalizika wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda 1994 hadi Novemba 2008, Kagame alipoamua kubadili mwelekeo na kuamua kumsaidia Rais Kabila kuwakabili Wahutu wa Rwanda waliojichimbia nchini Kongo.
Je, kukamatwa kwa Jenerali Nkunda ndio mwisho wa upinzani Mashariki ya Kongo? Tukae kimya tusubiri na tuone hali itakavyokuwa...Mungu Ibariki Afrika na watu wake!!!
No comments:
Post a Comment