Vitambulisho vya taifa
kutolewa mwaka huu
Serikali imesema vitambulisho vya Taifa vitaanza kutolewa rasmi mwaka huu na mchakato wa kumtafuta mkandarasi unatarajiwa kukamilika baada ya miezi minne kuanzia sasa. Pia katika hatua nyingine, imeahidi kufanya kila iwezalo kuhakikisha wauaji wa maalbino wanadhibitiwa, na hadi sasa watuhumiwa zaidi ya 100 wamekamatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, juu ya mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Nne, Waziri Lawrence Masha, alisema tayari michakato muhimu juu ya vitambulisho hivyo imekamilika.
“Tayari tumeshaunda Mamlaka ya Vitambulisho na itajulikana kama NIDA, ofisi imepatikana na Mratibu wa Vitambulisho, Dickson Maimu, ameteuliwa na vitambulisho vitaanza rasmi kutolewa mwaka huu,” alisema Masha.
Akizungumzia mauaji ya maalbino, Masha alisema hiyo ni moja ya changamoto ambazo zinaikabili wizara hiyo, kwani mauaji hayo ni aibu kubwa kwa Taifa hasa kutokana na dhana kuwa hufanywa kwa imani za kishirikina.
Alisema katika salamu zake za mwaka mpya, Rais Jakaya Kikwete, alisema kimeanzishwa kikosi kazi maalumu kilichojumuisha maofisa wa Polisi na wa Usalama wa Taifa, ili kufuatilia na kukomesha kabisa tatizo hilo.
Aliongeza pia kuwa wizara hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji katika kukabiliana na rushwa, imefukuza askari 44 na wengine kesi zao zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuendeleza juhudi za kutoa elimu juu ya athari za rushwa.
Alisema pia katika kipindi hicho, wizara ilikamata wahamiaji haramu 7,568, kati yao 5,712 walifukuzwa nchini na wengine 1,856 wanaendelea kuzuiwa katika magereza nchini wakisubiri kurudishwa kwao. Kuhusu siku saba alizotoa kwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, kutokana na madai ya kutishiwa kuuawa, alisema hadi sasa Mengi hajawasilisha ushahidi.
“Nilitoa siku saba kwa Mengi, alete uthibitisho aliosema anao kuhusu vitisho vya kuuawa, hakuleta, ieleweke kuwa wizara yangu inafanya kazi kwa kuchunguza ushahidi, na dhamira yake ni kulinda mali na maisha ya Watanzania, ila DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai) anaendelea na uchunguzi, mtaambiwa nini kinaendelea,” alisema.

No comments:
Post a Comment