Friday, January 09, 2009

Vunja mbavu (simu za mkononi)


TICHA MSELA, DENTI MSELA!

Mwalimu mmoja msela alikutana na mwanafunzi ambaye ni mtoto wa kijiweni aliyezoea kuongea lugha ya kihuni na maongezi yao yakawa hivi:

Denti: Oyaa ticha eeh! Nina swali mwana linanitesa kinoma, unaweza kunisaidia?

Ticha: Swali gani kichaa wangu?

Denti: Mwanangu nitonye kirefu cha V.V.U maana kuna mshikaji ananisumbua kweli na mimi wala sijui.

Ticha: Hilo mbona simpo tu kichaa wangu kama kumsukuma mlevi vile. V.V.U maana yake ni Vaa Vizuri Upendeze.

Denti:Duh! Hiyo kali...

Toka: Global Publishers Tanzania

No comments: